Virusi vya ukimwi ni vijidudu vinavyoshambulia mfumo wa kinga wa binadamu. Virusi hivi huathiri binadamu tu. Pindi virusi vya ukimwi vinapoingia katika mwili wa binadamu huanza kuzaliana na kuwa vingi. Ukimwi ni kifupisho cha maneno yafuatayo: “Upungufu wa kinga mwilini”.

Baada ya mtu kushambuliwa na virusi vya ukimwi kwa muda mrefu mwishowe Mfumo wa kinga ya mwili hudhoofika na hivyo mtu huwa katika hatari ya kupata Magonjwa mengi nyemelezi kama vile kikohozi, kuharisha, kansa ya ngozi na mengineyo kiurahisi kabisa kwani Mfumo wa Kinga hauna tena uwezo wa kupambana dhidi ya vijidudu vya magonjwa. Hali hii ndiyo huitwa ukimwi.

Ni matumaini yetu kuwa umeelewa sasa nini maana ya virusi vya ukimwi na ukimwi.

Mambukizi ya virusi vya ukimwi
Virusi vya ukimwi huenezwa kutoka kwa muathirika kwenda kwa mwingine kupitia njia mbalimbali kama ifuatavyo:

1.) Tendo la ndoa / kujamiiana
Njia kubwa na ya haraka ambayo Ugonjwa huu huambukizwa ni kupitia ngono zembe.

Iwapo Mtu atafanya ngono isiyo salama na mtu mwenye maambukizi ya UKIMWI ni rahisi sana kuambukizwa kwani Virusi wapo katika majimaji ya ukeni. Vilevile msuguano wakati wa tendo la Ndoa huchangia kwa kiasi kikubwa michubuko midogomidogo ambayo hutoa damu na kusababisha maambukizi.

2.) Kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto
Mama muathirika wa Virusi vya Ukimwi anaweza kumwambukiza mtoto wake katika hali tatu:
i) Mtoto akiwa tumboni
ii) Wakati wa kujifungua
iii) Wakati wa kunyonyesha

3.) Kushirikia na vifaa vyene ncha kali
Kushirikiana vifaa vyenye ncha kali kama vile wembe, sindano, na mikasi katika kukatia viungo vya mwili kuna hatari kubwa ya maambukizi ya virusi vya ukimwi kutokana na kchanganyika kwa damu kati ya muathirika na Mtu mwenye afya njema.

4) Kuongezewa damu isiyo salama
Wakati mwingine hutokea kuwa mgonjwa amepungukiwa na damu na hivyo anahitaji kuongezewa damu.Iwapo mgonjwa ataongezea damu yenye maambukizi anaweza kuambukizwa moja kwa moja.

Dalili za ukimwi
Katika hatua za awali baada ya mtu kuambukizwa ukimwi hakuna dalili zinazojidhihirisha. Hivyo huwezi kumtambua mtu kuwa ni mwathirika katika hatua hii ila kwa Vipimo vya kitaalamu tu. Hii ni kwa sababu bado mfumo wake wa kinga mwilini haujadhoofishwa na virusi vya ukimwi. Kadri siku zinavyoendelea ndivyo mfumo wa kinga mwilini unavyodhoofika na hatimaye hufikia hali mbaya, ambayo mwili unakuwa hauna tena nguvu ya kuzuia magonjwa nyemelezi.
Miongoni mwa dalili za ukimwi ni:
· Kupoteza uzito wa mwili zaidi ya 10%
· Kuharisha mfululizo zaidi ya mwezi, Hali hii hutokea baada ya Virusi kushambulia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula.
· Utepe mweupe mdomoni
· Kikohozi cha muda mrefu
· Magonjwa ya Ngozi, mfano: Malengelenge, upele na kadhalika.

Mambo yanayofikiriwa kuambukiza ukimwi lakinihayaambukizi
Kutokana na hatari ya ugonjwa huu mara nyingi watu wamekuwa wakiwanyanyapaa Mgonjwa kwa hata mambo ya kawaida ambyo hayawezi kusababasha maambukizi. Mfano wa mambo hayo ambayo hayaambukizi ukimwi ni:
o Kushikana mikono na mgonjwa wa ukimwi
o Kukumbatiana
o Kushirikiana vyombo vya Chakula
o Kushirikiana choo

Athari za ukimwi
Ugonjwa wa ukimwi una athari nyingi sana kuanzia kwa mgonjwa, familia na kitaifa.
Athari za ukimwi kwa mgonjwa
· Huzuni
· Kifo
Athari za ukimwi kwa Jamii

· Kuongezeka kwa yatima
· Utegemezi, mgonjwa anakuwa tegemezi kwa ndugu na marafiki.
Athari za ukimwi Kitaifa
· Taifa linapoteza nguvu kazi
· Serikali hupoteza mamilioni ya fedha katika harakati mbalimbali za kupambana na ugonjwa huu wa ukimwi.

Tags:
About Author: Abdallah Hemedi