Maelewano katika mapenzi ni suala linalo kamilisha maisha halisi na maana halisi ya neno mapenzi.Watu wanaoishi kwa amani na furaha katika mapenzi yao wana nafasi kubwa sana ya kufikia malengo yao kama wapenzi kuliko wale wanaoishi katika uhusiano usiokua na maelewano. Familia zote zenye maelewano ndizo zenye mafanikio katika jamii zote.

Ingawa kutokuelewana ni sehemu ya maisha ya watu wote walio kwenye mahusiano, lakini kuna baadhi ya mambo yanaweza kuzingatiwa na kuufanya uhusiano wowote ule kujengeka na kuwafanya wapenzi walio katika uhusiano husika kutimiza ndoto zao.

Mambo ya kuzingatia kujenga uhusiano imara

Heshima
Heshima ndio msingi wa kwanza na imara katika kila kitu hata nje ya mahusiano, ila tunapokuja kwenye suala la uhusiano heshima ndio nguzo kuu kabisa, kama hakutakua na kuheshimiana katika uhusiano ni wazi kabisa suala la amani na upendo pia litakua ni hadithi kwa wapendanao walio kwenye uhusiano husika. Hivyo basi ili kuondoa migogoro katika uhusiano ni lazima wapenzi waheshimiane hata katika mapungufu waliyo nayo kwa kufanya hivyo watakua wamepiga hatua kubwa sana katika ujenzi wa uhusiano imara.

Uvumilivu
Uvumilivu ni suala kubwa ambalo kila mtu kwenye mahusiano anatakiwa kua nalo, na katika upendo au mahusiano anaependa anatakiwa kuwa mvumilivu katika kila kitu kuhusu mwenza wake. Lazima ukubali mapungufu ya mwenzako na kuyafanya kama mzigo wako, katika kulifanya hilo ni lazima kila mtu aweze kumvumilia mwenzake katika kila kitu bila kusimangana au kusemana vibaya.

Uwazi
Ni vyema kila mtu katika uhusiano awe muwazi kwa mwenzie, mahusiano mengi yanavunjika kutokana na kutokuepo uwazi kwenye uhusiano, ni vizuri kila mtu anapoona hali ya tofauti au mabadiliko yoyote kwenye mahusiano awe muwazi kwa mwenza wake ili wayaweke mambo sawa, tofauti na hivyo hakuta kua na kujengeka kwa uhusiano kama kila mtu atakaa kimya katika jambo linalo msumbua kutoka kwa mwenza wake hali hii ya kutokuepo kwa uwazi kunaweza kusababisha mmoja kati ya wapendanao kutafuta anachokikosa nje ya uhusiano na hivyo kusababisha usaliti ambao mwisho wake ni kuvunjika kwa uhusiano.

Kuelewana
Hakuna binadamu aliekamilika ni jambo ambalo wapenzi wote wanatakiwa kulielewa, na kwa kulielewa hilo ni vizuri kila tatizo likazungumzwa kwa kuelewana ili limalizike. Ili kuweza kulikamilisha ilo ni lazima wote wawili waelewane katika kila kitu kati yao.

Utayari
Utayari umebeba maana kubwa sana katika maisha ya mahusiano, ni lazima kila mtu awe tayari kufanya kila kitu kwa ajili ya mwenzake. Upendo wa kweli ni kujitoa kwa ajili ya mwenzako, katika utayari ndiko kwenye mapenzi ya kweli. Kila mmoja awe tayari kutoa muda wake kwa ajili ya mwenzake, suala la utayari linasaidia sana katika kujenga msingi imara wa uhusiano kati ya wapendanao.

Ingawa hakuna kanuni zinazoweza kuwaongoza watu kuishi bila kutofautiana, lakini ni muhimu kila mmoja kuhakikisha anakuwa mbali na vishawishi vyovyote vinavyoweza kusababisha kutokuelewana na ni vyema kwa kila aliye kwenye uhusiano atambue mambo hayo matano ili kuweza kujenga uhusiano ulio imara na wenye furaha siku zote.

Tags:
About Author: Geofrey Shao