Kiharusi ni kitendo cha baadhi ya viungo vya mwili kuwa na ganzi au kutojiweza kufanya kazi zake za kawaida. Hali hii husababishwa na ukosefu wa damu katika ubongo kwa muda wa masaa 24 ama zaidi ila wakati mwingine damu hushindwa kufika katika ubongo endapo mishipa ipelekayo damu kwenye ubongo ikiwa imepasuka. Kutokana na tatizo hili linaweza kupelekea athari mbalimbali kujitokeza kwa mgonjwa endapo hazitachukuliwa hatua za haraka kwa mgonjwa aliyekumbwa na ugonjwa huu.

Mambo yanayoweza kumpata mgonjwa endapo hatua za makusudi na haraka hazitachukuliwa dhidi yake ni kama yafuatayo:

 1. Viungo na hatimaye mwili mzima kupooza, kutokana na tatizo hili husababisha viungo vya mwili kupooza hali ambayo hupelekea mtu kupoteza uwezo na ufanisi wa utendaji kazi wake kwa ufanisi wake.
 2. Kupoteza kumbukumbu, hii ni kwa sababu ugonjwa huu unaukumba ubongo kwa kukosa damu kwa kiasi kikubwa ndio maana mtu huwa anapoteza uwezo wa kukumbuka kwani ubongo ndio nyenzo pekee inayohusika na mambo ya kumbukumbu
 3. Kupoteza uwezo wa kuongea vizuri, watu wengi wanaokumbwa na tatizo hili huwa wanapoteza uwezo wa kuongea vizuri na hata baadhi yao kutoongea kabisa kutokana na tatizo hili la kiharusi.
 4. Misuli kuwa dhaifu, ili mwili uweze kuwa mkakamavu hutegemea kwa kiasi kikubwa ushirikiano kati ya ubongo na viungo vya mwili kwa ujumla katika kuhakikisha kila kiungo kinakuwa katika ubora wake kwa mfano misuli.
 5. Woga kupita kiasi, hali hii inatokana na kitendo cha ubongo kushindwa kufanya kazi yake kwa sababu ya ukosefu wa damu hali ambayo humfanya mgonjwa kutotambua kitu gani kina athari ama hakina athari kwake.

Pia ugonjwa huu wa kiharusi (ama kwa kiingereza stroke) umegawanyika katika sehemu mbili kutokana na jinsi gani umetokea ugonjwa huu kama ifuatavyo:

 1. Kiharusi cha kuvuja damu ndani ya ubongo ama kwa kitaalamu huitwa( Haemorrhagic stroke) aina hii ya kiharusi hutokea mara baada ya kupasuka kwa mishipa midogo midogo ipelekayo damu katika ubongo.
 2. Kiharusi cha kukosa hewa katika ubongo ambacho kitaalamu hujulikana kama Ischemic stroke, aina hii ni maarufu sana kwa watu wengi wanaopatwa na tatizo la kiharusi chanzo chake huwa ni ukosefu wa hewa kunako katika ubongo kwa muda flani hali ambayo hupelekea baadhi ya viungo vya mwili kushikwa na ganzi au kushindwa kufanya kazi zake vizuri kama vile mkono, na miguu.

Lakini ugonjwa huu wa kiharusi husababishwa na mambo kadha wa kadha katika miili ya binadamu kama ifuatavyo:

 1. Shinikizo la damu la muda mrefu
 2. Mafuta (thrombosis)
 3. Kuganda kwa chembe nyekundu za damu (sickle cell)
 4. Kuganda kwa damu kwenye mishipa (embolus)
 5. Upungufu wa usafirishaji wa damu kwenye ubongo

Pia unaweza gundua ugonjwa wa kiharusi endapo zitajitokeza baadhi ya dalili katika mwili wako kama zifuatazo;
a.) Kuumwa na kichwa (cerebral haemorrhage)
b.) Kuwepo kwa historia ya ajali ya kichwa
Kwa upande mwingine ugonjwa huu unaweza kutibiwa kwa kutumia njia tofauti tofauti ila miongoni mwa njia hizo ni kama hizi hapa; Mgonjwa anaweza tibiwa kwa kupewa dawa za kuyeyusha mafuta mwilini kwani mafuta huwa ndio chanzo cha mishipa midogo midogo kupasuka kutokana na kubanwa katika kuta zake.

Pia ugonjwa hutibiwa kwa njia ya upasuaji wa neva, lakini njia hii huhitaji uangalifu wa hali ya juu sana ili kuepusha madhara kwa mgonjwa kama vile kupoteza uhai. Ni ukweli usiopingika kuwa ugonjwa huu umekuwa tishio kwa miaka ya hivi karibuni hii ni kutokana na watu wenyewe kupendelea kwa kiasi kikubwa matumizi ya bidhaa za viwandani zinazowekwa mafuta kwa kiasi kikubwa kama vile maandazi chapati na hata minofu ya samaki iliyopekiwa kuliko zile za asili suala ambalo hupelekea watu wengi kukumbwa na tatizo hili hususani wazee kuanzia miaka 40 na kuendelea kuliko vijana.

Tags:
About Author: Shaibu Namnimuka